Chorus
{ Njooni tuimbe, njoni tucheze
Njooni tufurahi, mbele zake Bwana
Piga makofi, piga vigelegele
Shangilieni Bwana leo asubuhi } *2
Verse 2
Sauti ya kwanza semeni aleluya
Sauti ya pili tumsifu Yesu Kristu
Sauti ya tatu na ile ya nne
Waseme pamoja milele amina
Verse 3
Wamama wote pigeni vigelegele
Wababa wote vinanda vipigwe sana
Pigeni filimbi ngoma na kayamba
Watoto wadogo hoye changamkeni
Verse 4
Mataifa yote njoni mbele za Bwana
Makabila yote simameni tuimbe
Nyanyukeni wote pigeni makofi
Shangwe na nderemo vifijo machezo
Verse 5
Bahari na vitu vyote viijazavyo
Milima mito na miti shangilieni
Ndege wa angani na warukeruke
Wanyama kondeni furahini sana
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.