SectionsExitNota Mpaka Mbinguni

Nota Mpaka Mbinguni

Ordinary TimeExit
Verse 1

Tumetafiti tukauliza, maandiko tukafunua

Kutambua watakatifu, wanafanya kazi gani Mbinguni

Chorus

|s1| Usiku na mchana, jioni na asubuhi

Kiangazi masika mpaka Mbinguninn|s2| Tutamsifu Mungu, tutamwimbia

Watunzi tutampangia nota mpaka mbinguninn|a| Tutamsifu Mungu, tutamwimbia

Watunzi Tutampangia nota mpaka Mbinguninn |t| Tutamsifu, waimbaji tutamwimbia, watunzintutampangia nota mpaka Mbinguni (waumini)nn|b| Tutamsifu Mungu, tutamwimbia

Watunzi tutampangia nota mpaka Mbinguni

Verse 3

Enyi wasomi tuambieni, wanasayansi tujibuni

Katika mambo ya mbinguni, nini kinafanyika duniani

Verse 4

Tumetambua kule mbinguni, hakuna kwenda ofisini

Wala kumbi za burudani, hata kilimo hakuna lakini

Verse 5

Kumbe furaha za dunia hii, ni upumbafu ni wazimu

Na anasa za maadili, sisi waimbaji tumeamua

Verse 6

Waamini wote furahini, makasisi shangilieni

Nanyi watawa jiungeni, kwa waimbaji hakuna matata

Verse 7

Upendo wake ni wa ajabu, fadhili zake za milele

Huruma yake ni amini, msamaha wake unashangaza

Comments

Sign in to join the conversation

Share your thoughts on this hymn with the community.