Nyumba Ya Roho
Mungu wangu nikujue mimi, Mungu wangu nikupende
Mungu nikutumikie, kisha niurithi ufalme Mbinguni * 2n(wewe) roho umenipa ee, (kisha) ukaihifadhi vizurin(yaani) ndani ya mwili ee (kwani) mwili ni nyumba ya roho
Ndiwe mungu peke yako, wa kuabudiwa ni wewe
Nishike kitakatifu siku hiyo siku yakonnisilitaje kabisa bure jina lako Mwenyezi
Ulimi wa mwili wangu usiiponze roho yangu
Niwaheshimu wazazi, ili nisiwasononeshe
Uhai wa binadamu niuthamini yani nisiuue
Kuiba nijiepushe, kusema uwongo niache
Mwili wangu usizini ndipo roho yangu itapona
Niepuke kutamani yote yasiyo mali yangu
Naye mwanamke asiye mke wangu yani sio wangu
Hapo ndipo nitakuwa nimeutumia vizuri
Mwili ulioiumbia roho ifike Mbinguni juu
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.