Chorus
Ona mnavyopendeza,
ona mnavyometameta x2
Wapenzi wana harusinmwende mkaishi salama x 2
Verse 2
Kwenye maisha ya ndoa,
kuna raha pia tabu,
mkiishi kwa upendo tabu na raha ni sawa.
Mpendane siku zote,
katika maisha yenu,
msiruhusu shetani kuvuruga ndoa yenu.
Watoto mtakaopewa,
muwatunze hao vyema,
kwani kufanya hivyo Mungu mtampendeza.
Mjenge familia bora,
yenye kuheshimu sala,
kwani kwa njia ya sala tunaongea na Mungu.
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.