Jiandae wiki nzima weka tayarinsadaka yako mkristu (toa kwa moyo safi)
Usitoe kwa uchoyo wala sadaka ya kuaziman{(jasho lako) umtolee Mungu alicho kupa hahitaji zaidi
(maana) Vitu vyote mali yake toa kwa ukarimu } *2
Ninaona hasara kutoa (nanung'unika)
Bwana ona mi nilivyo changanyikiwa
Mara nyingi naomba jirani (hapa kitini)
siyo yangu ni sadaka ya kuazima
Ninaona uchoyo kutoa (sadaka yangu)
ninaleta kidogo tena kwa uchungu
Mara nyingine sitoi kitu (nilicho nacho)
ninaficha sadaka yangu mfukoni
Ninaona aibu kubaki (ni wasiwasi)
nimeketi nao wengine wanatoa
Mara nyingine hata siendi (nimekimbia)
kanisani ninahepa michango nyingi
Wana baraka wanaotoa (kwa moyo ule )
wa Abeli wa Ibrahimu na Isaka
Bwana Mungu haipendi sadaka (yake Kaini)
wala yule Anania na Safira
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.