SectionsEntranceSikiliza Ni Mpendwa Wangu

Sikiliza Ni Mpendwa Wangu

Pentecostal,EasterEntrance
Verse 1

Sikiliza ni mpendwa wangu,

Ni mpendwa wangu tazama anakuja. X2

Chorus

Akirukaruka milimani, akichacharikanvilimani, mpendwa wangu ni kama paa,

Ni kama ayala tazama anakuja X2

Verse 3

Tazama tazama asimama,

asimama nyuma ya ukuta wetu,

anachungulia dirishani,

atazama kimiani anakuja.

Mpendwa wangu alinena,

yeye alinena akaniambia,

ondoka ewe mpenzi wangu,

ewe mzuri wangu ili uje zako.

Nitazame nitazame uso wako,

niisikie sauti yako,

maana sauti yako tamu,

ni tamu na uso wako ni mzuri.

Mpendwa wangu kweli ni wangu,

hakika ni wangu na mimi ni wake,

mpendwa wangu ulisha kundi,

ulisha kundi lake kwenye nyinyolo.

Hata jua lipungue kweli,

na vivuli vyote pia vikimbie,

unigeukie mpendwa wangu,

unigeukie ewe mpendwa wangu.

Comments

Sign in to join the conversation

Share your thoughts on this hymn with the community.