Chorus
{ Siku ile niliyokuita, uliniitikia,
Ukanifariji nafsi kwa kunitia nguvu
Nitashukuru kwa moyo wangu (moyo) wote
Mbele ya miu-ngu nitakui-mbia zaburin(Nami ) nitakusujudu nikilikabili
Hekalu lako takatifu, hekalu lako takatifu } *2
Verse 2
Nitalishukuru jina lako, kwa ajili ya fadhili zako
Na uaminifu wako, kwa maana umeikuza
Ahadi yako kuliko jina lako loten
Verse 3
Ingawa Bwana yuko juu, amuona mnyenyekevu
Naye amjua mwenye kujivuna tokea mbali
Nijapokwenda katika shida utanihuisha
Utanyoosha mkono juu ya hasira za adui
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.