Chorus
Siku ulipobatizwa ndugu yangu,
ulimkana shetani (shetani) na mabaya yake yote
Uliikiri imani takatifu,
utamtukuza mungu (Mwenyezi) na sheria zake zote
Ona leo ndugu yangu, tazama, umemgeuka Yesu Mungu wako
Umelivunja daraja la Yesu, umejenga la Shetani ndani yako
Verse 2
Umelivunja daraja lake Yesu, umemkana rafiki wa milele
Shetani umemuita aje kwako atawale nyumba yako ndugu yangu
Verse 3
Wewe umekuwa chanzo cha maovu, umelibeba bendera la shetani
Umekuwa kiberiti cha shetani, anachowashia moto wa maovu
Verse 4
Muogope Mungu wako, ndugu yangu, acha matendo maovu tenda mema
Uishi katika Kristu ndugu yangu, kama ulivyoahidi siku
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.