{Simulia sifa zake Mungu
Tangaza maajabu ya Mungu
Kwa viumbe vyote vya dunia} *2n{(Jama) Kweli Mungu ni mkuu
A-tawala mataifa kwa haki yeye kila analolitenda
Kwe-tu ni mapenzi yake Mwenyewe }*2
Tazama dunia ilivyoumbika inavyopendeza
Milima, mabonde, misitu, mito, maziwa na bahari
Mungu ameviumba vyote, hakika vinapendeza
Simulia sifa za Mungu, Mungu wetu wa ajabu
Tazama dunia ilivyoumbika inavyopendeza
Wanyama na ndege samaki wadudu na viumbe vyote
Mungu ameviumba vyote, hakika vinapendeza
Simulia sifa za Mungu, Mungu wetu wa ajabu
Tazama dunia ilivyoumbika inavyopendeza
Katuumba sisi wanadamu kwa sura na mfano wake
Mungu ameviumba vyote, hakika vinapendeza
Simulia sifa za Mungu, Mungu wetu wa ajabun
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.