Chorus
Sisi wana dunia tukumbuke maneno,
aliyosema Bikira Maria
Alipowatokea watoto wa Fatima,
Lucia Francis na Jacinta
Alisema tusali, tusali rosari, tupate amani
Na tuwaombee wale wakosefu wasio na mwombezi
Na wasiomwamini Yesu Mwokozi wamuamini ili waokoke
Verse 2
Mama yetu anahuzunishwa sana,
na matendo yetu maovu
Anajua adhabu yetu ijayo,
hivyo anaona huruma sana
Verse 3
Atusihi tuache dhambi kwa dhati,
tuache kumkosea Yesu
Tuyatubu makosa yetu yote,
ili Bwana atupatie amanin
Verse 4
Tusitende maovu na dhambi,
atusihi mama wa Yesu,
Tusimkasirishe tena Mungu,
asije tutupa motoni milele
Verse 5
Ibada ya moyo safi wa Maria,
tuizingatie daima,
Tupokee komunio takatifu,
kila Jumamosi ya kwanza ya mwezin
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.