SectionsExitTazama Mama Mwanao

Tazama Mama Mwanao

Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Marian,Christmas,Advent,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,LentExit
Chorus

Tazama Mama mwanao, atundikwa msalabani

Sababu gani hi-yo, mwanao kutiwa hatianin{ Uchungu, mama, uchung,u mama,

Uchungu mama kwa mwanao } *2

Verse 2

[ s ] Sioni kosa lolote, alilolitenda mwanangu

Mwanangu hakuwa na kosa, makosa hayo juu yenu

Uchungu, uchungu, uchungu sana kwa mwanangu *2

Verse 3

[ t ] Kutundikwa juu msalabani, sababu yake ukombozi

Atukomboe utumwani, tuwe wana wa ukombozi

Ni sisi, ni sisi, ni sisi mama wakosefu *2

Verse 4

[ s ] Mwanangu haikumpasa, kufa bure bila sababu

Mwanangu Mungu mtu pekee, kwake sioni kosa kwangu

Uchungu, uchungu, uchungu sana kwa mwanangu *2

Verse 5

[ t ] Kumbuka mama Maria, maneno ya mwanao Yesu

Nitakufa nitafufuka, na kwenda juu kwa Baba yangu

Ya nini, ya nini, ya nini mama huzuni hiyo

Comments

Sign in to join the conversation

Share your thoughts on this hymn with the community.