Tazama Ninakuja Kwako
Tazama ninakuja kwako (Bwana),
Niyafanye mapenzi yako
Mimi ninajitoa kwako,nnaja kwako Bwana nipokee x2
Nimesikia Bwana, sauti yako yaniita kwako,
Yaniita nije kwako ili nikakutumikie.
Na mimi sina budi, kuitika wito wako,
Maana kila siku mimi hukutafuta wewe.
Naja kwako Bwana, nimejawa na furaha tele,
Nafsi yangu yashangilia kwa kuikaribisha kwako.
Na moyo wangu Bwana unakutukuza wewe,
Maana wastahili sifa zote pia utukufu.
Tazama naja kwako, ninayaleta maombi yangu,
Na sala zangu zote ninakuomba uzipokee.
Unisamehe dhambi na maovu niliyoyatenda,
Ili mimi niwe tayari kukupa sadaka takatifu
Ninajitoa kwako kuyatenda mapenzi yako,
Kwa nguvu zangu zote, kwa mawazo pia kwa vitendo,
Unijalie heri, unipe Roho Mtakatifu,
Aniongoze mimi, nitimize ninayoahidi.
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.