Verse 1
Tumpende tumsifu Mungu wetu wa milele na hata milele
Tulisifu jina lake tukufu, na kulitangaza ulimwenguni
Chorus
{Tumsifu daima kwa heshima nyingi
Ni Mungu kweli nasi tumsujudie } *2
Verse 3
Duniani hapasimami, ni pahali pa kuiweka miguu yake
Mbinguni ndipo aketipo , akiwaangalia wanadamu
Verse 4
Azishikaye mbingu na mawingu, zikae imara zisidondoke
Aupimaye mchana usizidi, wala usiku usididimike
Verse 5
Ailindaye mimea ya jangwani, pasipo mvua wala maji mengi
Azifanyaye bahari zidumu, hayo maji yake yasikauke
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.