SectionsExitTuna Haki Kufurahiwa

Tuna Haki Kufurahiwa

Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Lent,Ordinary Time,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Ordinary TimeExit
Verse 1

Tuna haki kufurahiwa leo, manabii walivyoagua

Yatimia sawasawa na chuo Rabi yetu amejifufuan

Verse 2

Mayahudi husema kwa kiburi amekwisha, juzi tukamwua

Kaburile limetimiwa mhuri, jiwe zito hapana fungua

Verse 3

Mambo gani niambie Yahudi, Askari mbio wakimbia

Wana woga hao mjini warudi, kaza jiwe mhuri mpya tian

Verse 4

Yahudi we, bure mashauriyo, sawa mshale urushwao juu

Ukianguka afumwaye ni huyo, za kupata hila zako kuu

Verse 5

Mpumbafu we na Mungu kushindana, ukiwaza kumfunga kwa jiwe

Kaburini Rabi hayumo tena, iwo iwo kaamka mwenyewe

Verse 6

Rabi yangu kweli amefufuka, na hakika ya imani yangu

Nayo basi kwa Yahudi kushtuka, mfumba domo, kimya kwa uchungu

Comments

Sign in to join the conversation

Share your thoughts on this hymn with the community.