Chorus
Tutaishia kusema hii dunia mbaya (kweli) * 2
Mungu kaikamilisha bila kusahau kitu sasa
Dunia iweje mbaya kwa sababu ya walimwengu
Verse 2
Mungu kaumba dunia kwa mpango kamilifu
Kuhakikisha usalama kwa kila alichokiumba
Mazao yanastawi chakula kinatutosha, na mvuanzinanyesha sana kwa sababu ya upendo wake
Verse 3
Wapo walio fukara ambao hawajiwezi
Matajiri hawawasaidii japo wana uwezo
Pia mahospitalini hongo zimeshatawala
Pesa sasa zinatawala kuliko upendo wa Mungun
Verse 4
Viongozi maofisini wananyanyasa raia
Bila hongo hakuna kazi ubinadamu uko wapi
Dunia hii ya leo imetapakaa damu
Silaha za kutisha sana kutwa kucha zafanya kazin
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.