SectionsExitTuwatunze Watoto

Tuwatunze Watoto

Ordinary TimeExit
Chorus

Watoto wetu ni Baraka tu,

a tuwatunze watoto wetu,

hawataacha njia, Mwenyezi, kwa neema anayowajalia

(basi wapenzi) tulee watoto kwa mapendo,

(hivyo ndugu) tulee watoto kwa hekima nao waimarike

(ni baraka) tulee watoto kwa hekima nao waimarike.

Verse 2

Ni bahati kabisa tuliyojaliwa,

tujitolee kuwalea ipasavyo ha!

Na kuwafunza yaliyo mema kijamii

Verse 3

Kweli wengine wanahusisha watoto,

wadogo kwa mambo yasiyoeleweka ha!

Na kuwafunza yasiyofaa kijamii

Verse 4

Tusiwatese watoto Mungu asema,

acheni wote waje kwangu nawapenda ha!

Tuwafundishe yale yanayostahili

Verse 5

Na vile watoto uwaleavyo wewe,

usiwanyime haki zao uwalinde we!

Uwapende uwatunze uwatumikie

Comments

Sign in to join the conversation

Share your thoughts on this hymn with the community.