Verse 1
Mama Maria Mwombezi wetu,
mama wa neema na hu-ruma
Tusikilize Mama wa Yesu,
tusikilize wakosefu
Chorus
Twakuomba Mama Maria,
kwa Mwanao Mama tuombee
Sala zetu Mama Maria,
kwa Mwanao mama zifikishe
Nyoyo zetu Mama Maria,
zatamani kufika mbinguni
Verse 3
Mama Maria uliye mwema,
tuliza nyoyo zetu wanao
Tunaposhindwa tusaidie,
tusije baki katika gizan
Verse 4
Mama Maria twakuamini,
mama wa Mungu msaada wetu
Matumaini yetu ni kwako,
katika shida tusimamie
Verse 5
Mama Maria usituache,
umpelekee Bwana maombi
Atubariki wenye mashaka,
tupate uzima wa milele
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.