Utukufu juu kwa Mungu, Utukufu juu Mbinguni
Na amani kote duniani, Kwa wenye mapenzi mema
Tunakusifu tunakuheshimu, tunakuabu tunakutukuza
Twakushukuru kwa ajili, ya utukufu wako mkuu
Ewe Mungu ndiye mfalme, wa mbinguni Baba mwenyezi
Ewe Bwana Yesu Kristu, wa pekee mwana wa baba
Ewe Yesu mwanakondoo, wa Mungu mwana wa Baba
Ewe mwenye kuziondoa, dhambi zetu tuhurumie
Ewe mwenye kuziondoa, za dunia dhambi za watu
Ewe mwenye rehema nyingi, upokee maombi yetun
Uketiye kuume kwake, Mungu Baba tuhurumie
Kwa kuwa ndiwe uliye, peke yako Mtakatifu
Peke yako ni wewe Bwana, peke yako Bwana mkuu
Peke yako ni mkombozi, peke yako Yesu Kristun
Naye Roho Mtakatifu, katika utukufu wake
Mungu mmoja anayeishi, na kutawala milele yote.n
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.