Verse 1
Utukufu kwa Mungu, na amani duniani
Kwa watu wenye mapenzi mema
Kwa wenye mapenzi mema
Verse 2
Tunakusifu Bwana tunakuheshimu
Twakuabudu Bwana tunakutukuza
Twakushukuru Baba Mwenyezi mfalme wa Mbinguni
Verse 3
Ewe Bwana Yesu Kristu, mwana wa pekee
Mwanakondoo wa Mungu, mwana wake Baba
Uondoaye makosa yetu tuhurumie
Verse 4
Tunakusifu Bwana utusikilize
Wewe unayeketi kuume kwa Baba
Ni pekee Bwana ni mtakatifu mkuu Yesu Kristun
Verse 5
Pamoja naye Mungu, Roho Mtakatifu
Katika utukufu wake Mungu Baba
Milele yote milele yote amina amina
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.