Chorus
Utukufu kwa Mungu juu
Na amani duniani
Na amani kwa watu woten{Wenye - wenye mapenzi,
Watu - wenye mapenzi
Mema - wenye mapenzi
Watu - wenye mapenzi mema }*2
Verse 2
Tunakusifu tunakuheshimu
Tunakuabudu tunakutukuza
Tunakushukuru kwa ajili ya
Utukufu wako, wako mkuu
Verse 3
Ee Bwana Mungu mfalme wa mbinguni,
Mungu Baba mwenyezi ee Bwana Yesu Kristu
Mwana wa pekee ee mwana Mungu
Mwanakondoo wa Mungu, mwana wa Baba
Verse 4
Mwenye kuondoa dhambi za dunia
Ewe mwenye kuondoa dhambi za dunia
Pokea ombi letu ewe mwenye kuketi
Kuume kwa Baba, utuhurumien
Verse 5
Kwa kuwa ndiwe uliye peke yako
Peke yako mkuu ee Bwana Yesu Kristu
Pamoja na roho mtakatifu
Katika utukufu, wa Mungu Baba amina
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.