SectionsEucharistUtukufu (Misa Amecca)

Utukufu (Misa Amecca)

Ordinary TimeEucharist
Verse 1

Utukufu kwa Mungu juu mbinguni

Na amani kote duniani

(Kwa watu) wenye mapenzi mema

Chorus

n|s/a| Tunakusifu Baba, tunakuheshimu,

Twakuabudu sisi tunakutukuzan|t/b| Kusifu tunakusifu, heshimu,

Twakuabudu abudu tunakutukuza

Verse 3

Twakushukuru Mungu kwa ‘tukufu

Wako mkuu ewe Mungu mfalme

(Ee Baba) wa Mbingu Baba yetu

Verse 4

Bwana wetu mwokozi Yesu Kristu

Mwana wa pekee wake Mungu

(Uliye) Mwanakondoo wa Mungu

Verse 5

Unayeziondoa dhambi zote

Za dunia utuhurumie

(Pokea) pokea ombi letu

Verse 6

Wewe unayeketi kuume

Kwake Baba utuhurumie

(Sikia) sikia ombi letu

Verse 7

Kwani pekee yako ndiwe Bwana

Pekee yako mkuu na mkombozi

(Pekee) pekee Yesu Kristu

Verse 8

Kwa umoja wa Roho mtakatifu

Ndani yake Baba watukuzwa

(Ee Yesu) milele na milele

Comments

Sign in to join the conversation

Share your thoughts on this hymn with the community.