SectionsEucharistUtukufu (Misa Upendo)

Utukufu (Misa Upendo)

Ordinary Time,MarianEucharist
Chorus

[s] Utukufu kwa Mungu juun[w] Utukufu na amani duniani

Kwa watu wote wenye mapenzi

Kwa watu wote wenye mapenzinmapenzi mema (utukufu) *2

Verse 2

Tunakusifu tunakuheshimu,

Twakuabudu tunakutukuza

Tunakushukuru Mungu kwa ajili,

Ya utukufu wako mkuu

Ee Bwana Mungu, Mfalme wa Mbinguni,

Mu-ngu Baba, Mungu mwenye enzi,

Bwana Yesu Kristu, Mwana wa pekee,

Ee Bwana Mungu, ee Bwana Mungu

Verse 3

Mwanakondoo mwana wake Baba,

Uondoaye dhambi za dunia

Utuhurumie utuhurumie,

Pokea ombi letu ee Baba

Mwenye kuketi kuume kwa Baba,

tuhurumie utuhurumie

Kwa kuwa kwa kuwa, ndiwe peke yako,

mtakatifu mtakatifu

Verse 4

Pekee Bwana mkuu Yesu Kristu,

pamoja naye Roho Mtakatifu

Katika katika utukufu wake,

Mu-ngu Baba a-amina.

Comments

Sign in to join the conversation

Share your thoughts on this hymn with the community.