SectionsExitUzuri Wa Kifo

Uzuri Wa Kifo

Ordinary Time,MarianExit
Chorus

Basi ndugu zangu, hatimaye imetosha

Acheni kunung'unika kuhusu kifo

Jitayarisheni ili mfe kifo chema

Hiyo hekima ya kweli na ucha Mungu kamili

Kifo ni zawadi ya upendo toka kwa Mungu

Nacho kimeandaliwa kuivuka dunia chungu

Ibada na dini zenu ni upuuzi mtupu

Kama mwisho wake siyo kumfikia Mungu

Lakini hamuwezi kumfikia Mungu

Isipokuwa kwa njia hii ya kifon

Verse 2

Dhambi ya Adamu ilimfanya Adamu,

akajificha mbali na uso wa Mungu

Akapewa kifo,

kusudi roho yake irudi karibu na Mungu milelen

Verse 3

Kifo kilibeba maana yake halisi,

alipoinuliwa Mwokozi wa watu

Akashinda kifo,

kusudi watu wake baada ya kifo warudi kwa Mungu

Verse 4

Kama hampendi, taabu za ulimwengu,

kwa nini mwaogopa kujitayarisha

Kupokea kifo,

kusudi muiage dunia mpokee raha ya milele

Verse 5

Tofautisheni, kifo nayo mauti,

mauti humpeleka mwenzetu kuzimu

Ingawaje kifo,

humtenganisha mwenzetu na taabu za dunia hii

Comments

Sign in to join the conversation

Share your thoughts on this hymn with the community.