Chorus
{ Wakati sasa umeshafika wa kujifikiria
Kitu gani umtolee Bwana kama shukrani zako } *2n{ Toa kwa moyo wa mapendo,
Toa ulicho nacho (ndugu) toa kwa ukarimu
Mungu anakuona ndugu mpaka moyoni mwako } *2
Verse 2
Ewe ndugu usimame, nenda mbele zake Bwana
Kamtolee sadaka Bwana kwa mapendo yote
Verse 3
Tolea moyo wako, pamoja na matendo yako
Naye Bwana Mungu wako kweli atakubariki
Verse 4
Siku zote Mungu wako amekulinda vyema
Nawe sasa ndugu yangu hima ujifikirie
Verse 5
Baraka zake Mungu za Baba na za Mwana
Na za Roho Mtakatifu ziwe nanyi siku zote
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.