{Watu hawatalingana (daima), watatofautiana
(nayo ni) makusudi yake Mungu, jina lake litukuzwe } *3
{ Sote tumeumbika tulivyo (kadiri) ya mapenzi yake Mungu
Ili utukufu wake Mungu (Mwenyezi) ujulikane kwa wote } *2
Kweli wanadamu wote (hakika) tumeumbwa kwa udongo
(hivyo) asili yetu ni moja, tumetoka mavumbini
Wapo walio wanyonge (lakini), pia wapo wenye nguvu
(kusudi) Mungu kawaumba hivyo, ili wahudumiane
Wengine kawabariki (sana), amewajalia mali
(lakini) wengine amewashusha, wamekuwa hohe hahe.
Wale walio tajiri (kamwe), wasiwanyime fukara
(kwani) maskini wahitaji, huruma ya matajiri
Wote tu wana wa Mungu (hivyo) tuonyeshane upendo
(ili) Mungu wetu atukuzwe, sasa na hata milele.
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.