Chorus
{ Wewe Petro, nakwambia, utanikana mara tatu
Kabla ya jogoo kuwika, wewe Petro utanikana } *2
Verse 2
Simoni Petro akamwambi, Bwana unakwenda wapi
Yesu akamjibu, niendapo huwezi kunifuata sasa
Lakini utanifuata baadaye
Verse 3
Petro akamwambia, Bwana,
Kwa nini mimi siwezi kukufuata sasa
Mimi nitatoa uhai wangu kwa ajili yako
Verse 4
Yesu akamjibu, je wewe utautoa uhai wako kwa ajili yangu
Amin amin nakuambia wimbi hatawika
Hata wewe utakapokuwa umenikana mara tatu
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.